BOIPLUS SPORTS BLOG

ROMA YAMKANA FABREGAS

KLABU ya soka ya As Roma imekanusha taarifa kuwa kuna mazungumzo ya kutaka kumsajili kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas baada ya kukosa namba kwenye kikosi cha kwanza.


Kiungo huyo Mhispania mwenyewe uwezo wa kupiga pasi za uhakika amekua na hatihati ya kuondoka klabuni hapo lakini taarifa kutoka Sky Italia zinasema Roma inaanda ofa ya kumtoa Radja Nainggolan au Antonio Rudiger katika dili la kumpata Fabregas.


Kocha wa Chelsea Antonio Conte amekiri kuwa hana uhakika wa kiungo huyo kubaki Stamford Bridge kwa muda mrefu.
JUVENTUS KUMALIZANA NA AXEL

Timu ya Juventus 'Kibibi kizee' cha Turin ipo mbioni kumnasa kiungo raia wa Ubelgiji na klabu ya Zenit St Petersburg Axel Witsel.


Gazzetta dello Sport limeripoti kuwa mabingwa hao wa Italia wanakaribia kukubali dili la euro 6 milioni  kuweza kukamilisha saini ya Mbelgiji huyo ambapo walikaribia kunasa saini ya  kiungo huyo majira ya joto ila Zenit ikakataa ofa yao masaa 11 kuelekea kufungwa kwa dirisha la usajili.


Axel Witsel ambae mkataba wake utamalizika mwishoni wa msimu huu pia amekua akihitajiwa  na klabu ya Everton ya Uingereza.DORTMUND WASEMA PULISIC HAUZWI


Klabu ya Borussia Dortmund imewataka Liverpool kuachana kabisa na mpango wa kumsajili kiungo mshambuliaji wao Christian Pulisic.


Meneja wa michezo wa klabu hiyo Michael Zorc ametoa taarifa hizo za Liverpool kuachana na jitihada za kumpata kiungo huyo mwenye umri wa miaka 18 ambaye walimuhitaji tangu majira ya joto yaliyopita kabla ya kurejea tena kuhitaji saini yake kwenye dirisha lijalo la mwezi Januari.


"Tumeshasema na tunatilia mkazo kuwa hatupo tayari kumuuza Christian sababu tuna mipango nae na Liverpool hata wasijisumbue kutoa ofa" alisema Zorc. DELE ALLI ASEMA HAENDI POPOTE


Kiungo mshambulaiji wa Tottenham Hotspurs Dele Alli amesema atabaki katika jiji la London mbali na Paris Saint Germain kuhitaji huduma yake.


Dele anahusishwa na matajiri hao wa Ufaransa katika dili la paundi milioni 50 ili kwenda kukipiga katika ligi kuu ya Ufaransa 'League 1' baada ya kuonyesha kiwango bora.


Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 amekiri kuifikiria Spurs zaidi na kwa muda huu hafikirii kwingine zaidi ya kubaki jijini London.


 Alli alisema "ni fununu tu zisizo kuwa na uhalisia wowote, nimesaini mkataba mpya hapa na nina furaha kuwepo hapa na sifikirii mahali pazuri kwa umri wangu zaidi ya hapa" 

BONAVENTURA KUMRITHI FABREGAS CHELSEA

Vinara wa ligi ya Uingereza Chelsea wanafuatilia kwa ukaribu mkataba wa kiungo wa AC Milan Giacomo Bonaventura ili kuchukua nafasi ya kiungo Cesc Fabregas ambaye siku zake za kuishi Stamford Bridge zinasehesabika.


Kocha wa Chelsea Antonio Conte amekuwa akimkubali sana kiungo huyo kwa uwezo wake mkubwa na angependa siku moja ajiunge na vijana hao wa darajani.


Chelsea itatakiwa ofa ya euro milioni 23 ili iweze kupata saini ya kiungo huyo Muitaliano na kuziweka rehani ajira za Fabregas na Mikel Obi klabuni hapo.

Post a Comment

 
Top