BOIPLUS SPORTS BLOG

MANDZUKIC KUBAKI JUVENTUS

MSHAMBULIAJI wa Juventus raia wa Croatia Mario Mandzukic ameungwa mkono na Makamu wa  Rais wa klabu hiyo kuendelea kubakia na 'kibibi kizee' cha Turin.

Pavel Nedved ambaye ndiye makamu wa Rais wa Juventus amemfariji Mandzukic kutokana na taarifa kuwa mshambuliaji huyo hana furaha klabuni hapo huku akikasirishwa na kufanyiwa mabadiliko katika ushindi wa 3-1 waliopata dhidi ya Torino huku mshambuliaji huyo akikataa kushangalia pamoja na wenzake.

"Tumeishamaliza swala la mshambuliaji huyo na tumekuwa tukifanya vizuri huku tukiweka ushindani hapa Italia na tukipata matokeo mazuri," alisema Nedved 


LEWANDOWSKI HAENDI POPOTE

Miamba ya Ujerumani timu ya Bayern Munich hawapo tayari  kuwaachia mastaa wake kuondoka akiwemo mshambuliaji Robert Lewandowski hivyo wanaandaa ofa nono kwa ajili ya kuwabakisha nyota hao.

Lewandowski ambaye ni mshambuliaji tegemezi ameandaliwa ofa kubwa ya kumfanya abakie Allianz Arena na kusaini mkataba wa miaka minne taarifa zikitokea BILD chombo cha habari cha huko nchini Ujerumani.

Lewandowski anategemewa kusaini mkataba huo kabla mkataba wake haujaisha mwishoni wa msimu huu na kuikata maini timu ya Real Madrid iliyokuwa ikimuhitaji.ARSENAL WAMNYATIA LINGARD WA UNITED

Washika bunduki wa London timu ya Arsenal huenda wakafanya usajili wa kushangaza kwa kutaka kumnasa mshambuliaji Jesse Lingard wa Manchester United.

Taarifa kutoka Express zinasema Arsenal wanaona mazingira ya Lingard yanafanana na Danny Welbeck kipindi walivyomsajili kutoka kwa mashetani misimu miwili iliyopita. 

Welbeck alisajiliwa kipindi kiwango chake kiliposhuka na kuwekwa benchi mara kwa mara hivyo kocha Arsene Wenger huenda akatumia njia hiyo na kumpata Lingard mwezi Januari kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 10.


MOURINHO ANAMTAKA FONTE

Beki wa kati wa Southampton Jose Fonte huenda akatimka klabuni hapo mwezi Januari mara baada ya klabu hiyo kukataa kukidhi mahtaji ya mshahara mnono katika mkataba mpya.

Fonte alikaribia kutua United msimu uliopita ila hawakufikia makubaliano na hivyo beki huyo akabakia Southampton. Huenda Kocha Jose Mourinho akarejea na ofa nyingine mwezi ujao na kumnyakua nyota huyo.

Taarifa kutoka ESPN zinasema beki huyo wa kati raia wa Ureno atapatikana kwa paundi milioni 5 endapo klabu zinazomuhitaji zitatoa dau hilo katika dirisha dogo Januari.


VITGIL KUTUA MAN CITY

Klabu ya Manchester City ipo katika mipango ya kuboresha safu yake ya  ulinzi kwa kutaka kusajili  beki wa kati wa Southampton Virgil Van Dijk raia wa Uholanzi.

Van Dijk ambae amekua na kiwango bora msimu huu anatakiwa pia na  klabu kama Liverpool na Manchester United ambazo zimeonesha nia ya kuhitaji huduma yake. Kocha Pep Guardiola anapenda kupata beki wa kati aliye na nguvu na Van Dijk ndiye chaguo lake la kwanza.

City italazimika kutoa paundi  50 milioni kama walizomsajilia beki Jones Stones kutoka Everton msimu uliopita.

Post a Comment

 
Top