BOIPLUS SPORTS BLOG

www.boiplus.blogspot.com
MILAN YAMTAKA FELLAINI 

Miamba ya soka nchini Italia AC Milan imeonesha nia ya kumuhitaji kiungo Mbelgiji wa Manchester United Marouane Fellaini baada ya kutokuwa katika mipango ya kocha Jose Mourinho.

Mahasimu wao wakubwa Inter Milan pia wapo katika mbio za kugombea saini ya kiungo huyo ambaye  ameonekana akiwa nchini Italia na kaka yake huku kukiwa na habari za kuhusishwa na klabu hizo za jiji la Milan katika dirisha la usajili la mwezi ujao.

Fellaini amefunga mabao saba katika ligi kuu nchini Uingereza tangu ajiunge na Mashetani  hao  kwa ada ya uhamisho wa euro milioni 34 akitokea Everton.

LEIPZIG WAJIUNGA MBIO ZA KUMNASA DEMBELE

Vinara wa ligi kuu ya Ujerumani RB Leipzig wamejiunga katika orodha ya klabu zinavyohitaji saini ya mshambuliaji hatari wa Celtic Moussa Dembele.

Dembele ameivutia klabu hiyo iliyoanzishwa mwaka 2009 wakitaka kuboresha safu yao ya ushambuliaji ambayo kwa sasa inaongozwa na Werner ambaye ndio kinara wa mabao kwa klabu hiyo.

Leipzig ambao wametengeneza kikosi cha vijana chini ya meneja Ralph Hasenhuttl na meneja wa michezo Ralf Rangnick wamevutiwa na mshambuliaji huyo na kumfanya kuwa chaguo la kwanza kwenye usajili wa mwezi Januari ambapo watatatikiwa kutoa dau lisilopungua milioni 40.

DRAXLER KUTIMKA WOLFSBURG

Mshambuliaji wa Wolfsburg raia wa Ujerumani Julian Draxler amekiri kutaka kutimka Wolfsburg mara baada ya mechi dhidi ya Hertha Berlin waliokubali kichapo cha mabao 3-2.

Winga huyo alishuhudia mashabiki wa Wolfsburg wakimzomea katika mechi hiyo baada ya kuingia akitokea katika benchi ambapo alikiri kuwa anaangalia uwezekano wa kutimka klabuni hapo katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari.

Draxler amekua akihitajiwa na Arsenal kwa muda mrefu huku klabu za Tottenham,Liverpool na Juventus zikiingia katika mbio za kumnasa.


MADRID YAKARIBIA KUMNASA WEIGL

Real Madrid wapo katika nafasi nzuri ya kuinasa saini ya kiungo mkabaji wa Borussia dortmund Julian Weigl.

Kufuatia makubaliano ya  Madrid na Dortmund katika kuuziana haki ya kwanza ya mchezaji imewafanya miamba hiyo ya Hispania kuwa karibu zaidi kumnasa kiungo huyo raia wa Ujerumani.

Kocha wa Madrid Zinedine Zidane anataka kufanya  maboresho katika nafasi ya kiungo mkabaji baada ya Casemiro kukosa mtu wa kumsaidia katika nafasi hiyo.

REUS KUMRITHI SANCHEZ ARSENAL

Kiungo mshambuliaji wa Borussia Dortmund Marco Reus amekuwa chaguo la kwanza kwa klabu ya Arsenal kwenye la usajili endapo Alexis Sachez ataamua kutimka.

Winga huyo ambaye amekuwa na uwezo mkubwa  uwanjani mbali na kuwa na majeruhi mara kwa mara amemvutia kocha Arsene Wenger na kuwa chaguo la kwanza  katika wachezaji atakaowasajili ili kuboresha kikosi chake.

Arsenal watalazimika kutoa ofa isiyopungua paundi milioni 50 ili  kuishawishi  Dortmund kumwachia nyota huyo ambaye ni miongoni mwa wachezaji muhimu klabuni hapo.

Post a Comment

 
Top