BOIPLUS SPORTS BLOG

www.boiplus.blogspot.com
TURAN NAE KUELEKEA CHINA

Kiungo mshambuliaji wa Barcelona Arda Turan amehusishwa na uhamisho wa kuelekea nchini China ambapo wanandinga wanalipwa pesa nyingi.

Turan ambae alikataa ofa ya kujiunga na Arsenal majira ya joto yaliopita na hivyo kubakia Barcelona kugombania namba na kupata dakika nyingi za kucheza.

Turan ana husishwa na ofa ya euro milioni 50 kuelekea katika klabu zinazoshiriki ligi ya China.JAMES HAONDOKI REAL MADRID  

Wakala wa kiungo mshambuliaji wa Real Madrid James Rodriguez Jorge Mendes amesema mchezaji huyo hatotimka klabuni hapo katika kipindi hiki.

James  ametengewa ofa kutoka klabu za mbali mbali kutoka ligi kuu nchini Uingereza alikuwa anategemea kutimka mwezi January huku Chelsea ikionekana kuwa mstari wa mbele kupata saini ya raia huyo wa Colombia.

Madrid wameweka wazi thamani ya mkataba aliobaki huku wakala wake akithibitisha kuwa atampigania kiungo huyo kubaki na kufanikiwa kisoka klabuni hapo.

ZAHA KUJIUNGA NA SPURS

Winga wa Crystal Palace Wilfred Zaha anakaribia kutua Tottenham Hotspurs mara baada ya klabu hiyo kuandaa ofa nyingine ya kumnasa mwezi ujao.

Tottenham ambao walituma ofa ya paundi milioni 12 ilikataliwa na Palace hivyo kuwafanya wajiandae na ofa kubwa zaidi ya paundi milioni 30 itakayoweza mnyakua winga huyo.

Zaha amekua katika msimu bora na Palace chini ya aliyekua kocha wao Alan Pardew aliyetimuliwa siku chache zilizopita.BARCELONA KUMSAJILI CANCELO

Klabu ya Barcelona imeendelea na mchakato wa kumsajili beki Joao Concelo kutoka Valencia ili kuziba nafasi ya beki wa kulia iliyoachwa na Dani Alves aliyetimkia Jeventus majira ya joto yaliyopita.

Cancelo amekuwa katika orodha ya wachezaji wanaotakiwa na miamba hiyo ya Hispania majira ya joto ya mwaka 2017 ambapo Barcelona wamekua wakimfuatilia kwa takribani miezi mitatu hadi sasa.

Inavyoelekea Barcelona hawana budi kukubali kutoa ofa ya euro milioni 30 ambayo Valencia wanahitaji ili kumwachia beki huyo.

Post a Comment

 
Top