BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu

MSHAMBULIAJI Zahoro Pazi aliyesajiliwa Mbeya City amemtumia ujumbe mfupi wa maneno (SMS) Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi akimuomba kumsaidia ili apate ITC yake inayoshikiliwa na timu ya FC Lupopo ya DR Congo.

Endapo Pazi atashindwa kupata ITC hiyo itakuwa vigumu kucheza mechi za Ligi Kuu Bara ambapo kesho Jumamosi City wanaikaribisha Kagera Sugar na yeye huenda akakosa mechi hiyo.


Katika ujumbe huo, Pazi alikwenda mbali zaidi kwa kumueleza Malinzi kuwa suala lake linafahamika huku akidai kuwa mchezo mzima ulichezwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura aliyetoa kibali chake kwenda Lupopo na sasa TFF haimpi ushirikiano wa kupata kibali hicho.

Post a Comment

 
Top