BOIPLUS SPORTS BLOG


UKUNGU mzito uliotanda uwanjani wakati wa maandalizi ya mchezo kati ya wenyeji Sassuolo na KRC Genk umesababisha mechi hiyo ya kukamilisha ratiba ligi ya Europa kuahirishwa hadi kesho.

Hali hiyo ya ukungu ilikuwepo tangu jana wakati wa mazoezi ya mwisho ya Genk ambapo mtanzania Mbwama Samatta anayechezea Genk aliiambia BOIPLUS kuwa ilikuwa vigumu hata kumuona mtu aliye mita 10 kutoka aliposimama.

Kutokana na hali hiyo mchezo utapigwa kesho majira ya saa 2:30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki katika dimba la Stadio Cittá del Tricolore.

Mechi hiyo ni ya kukamilisha ratiba tu kwani tayari katika kundi F Genk na Athletic Bilbao zilishafuzu huku Bilbao wakimaliza vinara na pointi zao 10 kabla ya mchezo wa kesho ambao Genk ikishinda ama kupata sare itaongoza kundi.

Post a Comment

 
Top