BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar
James Kotei katikati akiingia uwanjani kuichezea Simba kwa mara ya kwanza

KIUNGO mpya wa Simba Mghana, James Kotei amewatuliza mashabiki wa timu hiyo kuwa kipigo walichokipata dhidi ya Mtibwa Sugar kisiwakatishe tamaa ingawa amesema mechi hiyo haikuwa ya kupoteza.

Jana Jumatatu, Simba walicheza mechi hiyo ya kirafiki iliyopigwa Uwanja wa Chamazi na kufungwa bao 2-1.

Kotei ameiambia BOIPLUS kuwa hajajisikia furaha kupoteza mechi hiyo ila mashabiki watambue kuwa katika mechi matokeo kama hayo ni ya kawaida lakini amesisitiza kutoruhusu makosa yaliyofanyika kwenye mechi hiyo yajirudie wakati wa ligi hasa mzunguko wa pili unaoatarajia kuanza wikiendi hii.

"Mtibwa Sugar wamecheza vizuri hata sisi ila matokeo haya yametokea katika hali ya mchezo tu hatukuwa na sababu za msingi kupoteza mechi hii, nimejisikia vibaya ila tunawaahidi mashabiki wa Simba watafurahi.

"Kufungwa kwenye mechi ya kirafiki si kwamba Simba watashindwa kutwaa ubingwa nina imani kubwa ubingwa tutatwaa. Wachezaji, mashabiki na viongozi wasikatishwe tamaa na matokeo haya tupambane mwanzo mwisho," alisema Kotei.

Kiungo huyo ambaye ni mara yake ya kwanza kucheza soka hapa nchini alishangazwa na umati wa mashabiki waliofika kushuhudia mechi hiyo.

"Ghana huwezi kukutana mashabiki wengi wamekuja kuangalia mechi ya kirafiki, inaonyesha hapa mashabiki wanapenda soka na timu zao," alisema Kotei.

Post a Comment

 
Top