BOIPLUS SPORTS BLOG

NEW DELHI, India
BONDIA wa Tanzania  Francis Cheka amepoteza pambano lake raundi ya tatu usiku wa kuamkia leo kwa Technical Knockout (TKO) dhidi ya Vijender Singh la (WBO) uzito wa kati lililofanyika Thyagaraj mjini New Delhi.

Singh alimdhibiti Cheka kuanzia dakika ya kwanza ya pambano hilo kwa kumshushia makonde mazito ambayo alishindwa kuyahimili.

Singh kwa ushindi huo amefanikiwa kutetea taji lake la WBO Asia Pacific uzito wa kati na huu utakuwa ushindi wa 7 kwa TKO na ushindi wa nane tangu alipoanza kuzipiga ngumi za kulipwa.


Singh kwa mara ya kwanza alikuwa anakabiliana na mpiganaji mwenye rekodi nzuri na aliyepigana mapambano mengi alimmudu Cheka ambaye ni bingwa wa zamani wa dunia.

Cheka ambaye ni bingwa wa World Boxing Federation (WBF) Super Middleweight ameshinda mapambano 32 kati ya 43 na katika ushindi huo amewatandika kwa TKO mara 17 kabla  yeye kupigwa usiku wa kumkia leo kwa TKO.

Post a Comment

 
Top