BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu

MCHEZO wa fainali ya michuano ya  BOIPLUS  X-MAS CUP yaliyoandaliwa na kituo cha kukuza na kulea vipaji vya vijana cha Viyosa ulichezwa jana Jumatano ambapo timu ya Viyosa imefanikiwa kutwaa ubingwa huo na kujinyakulia kitita cha Sh 150,000.

Viyosa ilitwaa ubingwa huo kwa kuifunga Boma FC bao 2-1 mechi iliyochezwa Uwanja wa Mongera visiwani Ukerewe.

Boma ndiyo ilikuwa ya kwanza kutikisa nyavu za wapinzani wao dakika ya 43 bao lililofungwa na Vincent Julius huku Viyosa ikisawazisha dakika ya 52 kupitia mshambuliaji wao Hamady Tungaraza 'Madizo' wakati bao la pili na la ushindi likifungwa na Boniface Mashaka.

Kwa matokeo hayo Boma wameshika nafasi ya tatu na kunyakuwa Sh 100,000 huku Yosso ikishika nafasi ya tatu kwa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya UDC wakiambulia zawadi ya Sh 50,000, awali timu hizo zilitoka sare ya bao moja.


Mfungaji bora, Hamady Tungaraza akikabidhiwa zawadi yake na mkuu wa polisi wilaya ya Ukerewe, Jumanne Mkalipa

Zawadi ya Mfungaji Bora ilikwenda kwa Tungaraza kutoka timu ya Viyosa aliyepata Sh 25,000.

Akizungumzia udhamini huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Boi Investment inayomiliki mtandao wa BOIPLUS, Karim Boimanda alisema kuwa; "Jitihada zinazofanywa na Emily Mugeta ni kubwa sana, ndio maana tuliona ni vema tukamuunga mkono kwa kudhamini michuano hii iliyoandaliwa na kituo chake. 

"Pia vipaji vingi vinapotea huko vijijini kwavile hakuna anayeviona tofauti na huku mjini, sisi tutaongeza nguvu zaidi na tunapanga kudhamini michuano mingine mikubwa zaidi mwakani. Tumeanza na fedha kutokana na ufinyu wa muda ila udhamini ujao utakuwa mnono zaidi kwani tutatoa vifaa kwa ujumla," alisema Boimanda.

Post a Comment

 
Top