BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu, UKEREWE
TIMU ya Viyosa imetinga fainali ya michuano ya BOIPLUS  X-MAS CUP kwa kuifunga Yosso kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika dakika 90 za kawaida kwenye uwanja wa Mongera uliopo visiwa vya Ukerewe jijini Mwanza.

Severine Constantine aliifungia Yosso bao la kwanza dakika ya saba kabla ya Abdallah Twaha kusawazisha kwa mkwaju wa penalti dakika ya 13.Hamadi Tungaraza 'Madizo' aliifungia Viyosa bao la pili dakika ya 32 huku Emmanuel Humba akiisawazisha Yosso dakika ya 60 na kupelekea mchezo huo kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti.

Viyosa itacheza na mshindi kati ya UDC na Boma FC ambao watakutana kesho kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili itakayofanyika kwenye uwanja huo saa 10 jioni.

Fainali ya michuano hiyo inayodhaminiwa na mtandao wa michezo na burudani wa BOIPLUS itafanyika Disemba 28 kwenye uwanja huo saa 10 jioni.

Post a Comment

 
Top