BOIPLUS SPORTS BLOG

ANCELOTTI AMWAGIA SIFA MULLER
KOCHA wa Bayern Munich Carlo Ancelotti amemsifu mshambuliaji wake Thomas Muller baada ya kuonesha soka safi kwenye ushindi ugenini dhidi ya Mainz 05 baada ya kutoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Muller alitengeneza bao la pili lililofungwa na Arjen Robben na kuwafanya Bayern kukwea kileleni baada ya kufikisha pointi 30 sambamba na RB Leipzig huku Leipzig ikiwa na mechi mkononi dhidi ya Schalke 04 itakayopigwa leo.

"Muller alicheza vizuri sana daima nasema ni mchezaji mzuri ana uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali za mbele pia anauwezo mkubwa wa kubadili nafasi yake uwanjani timu ilicheza kwa  uelewano mzuri licha yakuwa mechi ngumu ila tumepata pointi tatu" alisema Ancelotti.

Bayern ilitanguliwa kufungwa baada ya Jhon Cordoba kuipatia goli la kuongoza Mainz dakika ya 4 ya mchezo lakini Robert Lewandowski aliifungia Bayern Munich mabao mawili na Robbeangaliakutaza


NAPOLI WAMTAKA BALOTELLI
Baada ya timu ya  Napoli kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Inter Milan, Kocha mkuu wa klabu hiyo Maurizio Sarri amefungua milango katika usajili wa Mshambuliaji wa mtukutu wa Nice Mario Balotelli.

Balotelli ameanza msimu vizuri baada ya kupachika magoli 7 katika mechi 9 akiwa na klabu yake mpya ya Nice.Balotelli alikua mmoja ya washabiki walioenda kutazama mechi kati ya Napoli dhidi ya Inter Milan.

"Inategemea na yeye ni vyema kuishi Nice lakini ni raha zaidi kuishi Naples. Mario ni mchezaji mwenye sifa sahihi kwa ajili ya timu yoyote na asipofiti basi ujue ni tatizo lake binafsi sijihusishi na mambo ya usajili ila kama akitaka kuja naweza mtumia namba ya meneja wetu Giuntoli" Sarri aliiambia Sky Sport Italia.

DEMBELE KUMRITHI COUTINHO LIVERPOOL
Kufuatia majeraha ya mda mrefu ya wachezaji Danny Ings na Philipe Coutinho huenda Liverpool ikamfungia kazi mshambualiaji wa Celtic Moussa Dembele kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi Januari.

Kocha wa majogoo hao wa anfield Jurgen Kloop anatazamiwa kuongeza mtu katika idara ya ushambuliaji ambapo Dembele anapewa nafasi kubwa ya kusajiliwa huku mshambuliaji Sadio Mane akikaribia kuikacha timu hiyo  kwenda kuisaidia timu yake ya taifa ya Senegal katika mashindano ya AFCON.

Liverpool itaanda kitita cha paundi milioni 20 ikiwa 10 kwanza na 10 nyingine baada ya kuonesha uwezo wake uwanjani kwa mujibu wa makubaliano. 

Dembele ambae alijiunga mwezi juni na Celtic ameonesha uhodari wake wa kucheka na nyavu baada ya kufunga mabao 17 katika michezo 27. 
Post a Comment

 
Top