BOIPLUS SPORTS BLOG

ROBERTO CARLOS AUTAKA UKOCHA AUSTRALIA
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil Roberto Carlos amefungua milango ya kutaka kufundisha soka katika timu inayoshiriki ligi ya Australia.

Carlos aliwahi kuzitumikia timu za  Belediyespor, Sivasspor za Uturuki na Anzhi Makhachkala ya Urusi katika nafasi ya ukocha.

Akiwa na furaha kuwa balozi wa Real Madrid Mbrazil huyo mwenye umri wa 43 alisema " kwanini isiwe? kila kitu kinawezekana katika soka hapa Madrid najifunza na ipo siku nitapata nafasi na ningependa siku nikirejea hapa  niwe kocha mkuu".


WENGER ASEMA WEST HAM WANA MIAKA MIWILI YA KUKAA SAWA

Kocha wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger ametoa kauli kuwa timu ya West Ham United huenda ikawachukua miaka miwili kuweza kupata matokeo mazuri kwenye ligi kuu nchini Uingereza.

Meneja huyo amesema hayo baada ya timu yake kuwabugiza 'Wagonga nyundo' hao wa jiji la London mabao 5-1 wakiwa nyumbani kuwapeleka katika nafasi ya 17 katika msimamo wa ligi.

Wenger alinukuliwa akisema "inachukua mwaka au miaka miwili kuwa vizuri zaidi mashabiki walikua upande wao wanatakiwa kutengeneza upya kitu kingine cha kuwafanya wachezaji waweze kujiamini na kujua kuwa wanacheza nyumbani".


MASHABIKI WALALAMIKIA RAFU YA AGUERO

Baada ya Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero kumchezea rafu mbaya beki wa kati wa Chelsea David Luiz mashabiki nchini Uingereza wamelaani tukio hilo.

Mashabiki hao walisema kama tukio hilo lingekuwa limefanywa na Diego Costa basi dunia nzima ingetaka haki itendendeke juu ya faulo hiyo ila kwa vile ni Aguero wanahisi ni jambo dogo ambalo linaweza kumalizwa juu juu.

Aguero ana historia ya kucheza rafu ya aina hiyo ambapo mwaka 2013 alimchezea tena Luiz kama alivyofanya katika mchezo wa juzi tofauti ni kwamba amepata adhabu ya kufungiwa mechi 4.KANE KUSTAAFIA SPURS

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Harry Kane amekiri kutaka kumalizia soka lake akiwa White Hart Lane baada ya kusaini mkataba mpya klabuni hapo utakao muweka hadi mwaka 2022.

Kane ameona hakuna sababu  zitakazomzuia kutofanikiwa jambo ilo kama klabu yake itaendelea kumhtaji. Mshambuliaji huyo baada ya kukusaini mkataba huo aliisadia Spurs kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Swansea City huku mwenyewe akitufunga mabao mawili.

Muingereza huyo ana mabao 5 katika mechi nne za mwisho alizocheza.

Post a Comment

 
Top