BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar

MSHAMBULIAJI wa Prisons, Jeremiah Juma anasumbuliwa na jeraha la goti ambapo sasa atalazimika kukaa nje ya uwanja hadi msimu ujao huku yeye akitamka kuwa atafata masharti ili akirudi uwanjani awe fiti kabisa.

Jeramiah aliumia timu yake ilipocheza dhidi ya Mbeya City wakati wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom, mechi iliyomalizika kwa sare tasa.

Akizungumza na BOIPLUS, Jerry alisema kuwa anaamini atarejea kikosini huku akiwa mwenye ari mpya ingawa timu yake bado haijapata mbadala halisi anayeweza kutikisa nyavu kama ilivyokuwa kwa straika huyo aliyefunga mabao 15 msimu uliopita.

"Nipo Mbeya lakini bado sitaweza kucheza mechi zilizobaki za ligi, nitakaa nje hadi msimu ujao ili nipone kabisa, naamini nitapona na kurejea uwanjani," alisema Jerry ambaye sasa ni mwajiriwa Jeshi hilo la Magereza.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Prisons, Oswarld Morris alisema kuwa; "Ni pigo kwetu na kwake maana linamrudisha nyuma kijana ila hatuna haraka naye acha apone tunaamini msimu ujao atakuwa amepona kabisa.

"Hatuwezi kuharakisha kumrejesha mchezaji uwanjani wakati hajapona vizuri, majeraha ya goti nayaelewa ni lazima afuate masharti, kwasasa kuna wachezaji wanaocheza nafasi yake ila bado mbadala wake hatuna," alisema Moris.

Post a Comment

 
Top