BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar

KIUNGO wa Simba, Mghana James Kotei amekiangalia kikosi cha Yanga kilipocheza na Azam FC juzi Jumamosi na kutamka neno moja kuwa watashinda mechi yao ya kesho Jumanne dhidi ya watani zao.

Simba na Yanga wanakutana katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi itakayochezwa Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.

Katika mechi ya juzi, Yanga ilishindwa kutamba mbele ya Azam ambapo iliambulia kipigo cha mabao 4-0 matokeo ambayo yamewapa jeuri Simba na kuiona ni kama mechi nyepesi kwao baada ya wao kushinda bao 2-0 dhidi ya Jang'ombe Boys.

Akizungumza na BOIPLUS, Kotei ambaye ni mechi yake ya kwanza dhidi ya Yanga alisema kuwa aliwaona wapinzani wao hao na hivyo anafahamu jinsi gani atakabiliana nao na kikubwa ni kihakikisha kwa umoja wao wanaipa Simba ushindi utakaofanya watinge fainali.

"Nimeona mashabiki wa soka huku wanapenda timu zao, nimefuatilia na kuambiwa hii ni mechi yenye upinzani mkubwa kutokana na historia ya hizi timu japokuwa kabla sijaja sikuwahi kubahatika kuiona hata moja.

"Kikubwa ninachoamini ni kwamba tutapambana na wenzangu kuhakikisha tunashinda mechi hiyo, Mungu atatusaidia," alisema Kotei.

Kotei alitua Simba baada ya ushawishi mkubwa wa rafiki yake Daniel Agyei aliyetokea Medeama ya Ghana na hii kwake itakuwa ni mechi yake ya kwanza kusimama langoni dhidi ya watani hao ingawa aliwahi kuwa langoni timu yake ya zamani ilipocheza na Yanga kwenye mechi za michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho hatua ya makundi na kutoka sare Uwanja wa Taifa.

Post a Comment

 
Top