BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar

KIUNGO wa zamani wa Azam FC, Jean Babtiste Mugiraneza 'Migi' ametoa siri yake kubwa katika soka lake kuwa enzi hizo alikuwa hapendi kucheza soka akiwa amevaa viatu wakati huo anacheza soka la mtaani maarufu kaka Chandimu.

Migi ambaye amejiunga na Gor Mahia baada ya kuvunja mkataba na Azam alianza kubadilika aliponunuliwa viatu vya kuchezea mpira na mshambuliaji wa zamani wa APR, Miri Hassan ambaye kwasasa hachezi tena kwani alistaafu. 

Migi tayari amejiunga na Gor Mahia na leo usiku watasafiri kwenda Sudan kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Al Hilal mechi itakayopigwa keshokutwa Jumapili na hiyo itakuwa mechi yake ya kwanza.

Kiungo huyo ameiambia BOIPLUS kuwa anafurahia maisha mapya ya Gor Mahia ambapo amepewa jezi namba saba aliyodai kuwa ni namba anayoipenda tangu alipoanza kucheza soka ingawa akiwa Azam aliikosa kutokana kwamba tayari Kelvin Friday alikuwa akiitumia.

"Napenda namba saba kwasababu ya Miri aliyeninunulia viatu vya michezo nikiwa mdogo kwani nilikuwa nacheza mpira mtaani bila viatu, hivyo nilianza kumpenda hadi namba hiyo aliyokuwa akiitumia yeye maana alichangia mimi kufika hapa nilipo sasa kwa kuninunulia kiatu kwa mara ya kwanza.

"Nilikuwa sijazoea kuvaa viatu wakati wa kucheza kwani nilikuwa na umri mdogo wakati huo nacheza tu mtaani. Nilipofika Azam sikuikuta namba ninayopenda ndiyo maana nilipewa namba 16," alisema Migi.

Post a Comment

 
Top