BOIPLUS SPORTS BLOG

Mshambuliaji Riyad Mahrez jana usiku alitangazwa kuwa mchezaji bora wa Afrika mwaka 2016 kwenye tuzo za CAF zilizofanyika Abuja nchini Nigeria

Kipa wa Mamelod Sundowns na timu ya taifa ya Uganda Denis Onyango akatwaa tuzo hiyo ila kwa wachezaji wanaocheza barani Afrika. Tuzo hii ilikuwa ikishikiliwa na mtanzania Mbwana Samatta ambaye alitimkia nchini Ubelgiji katika klabu ya KRC Genk

Nyota wa Nigeria, Kelechi Iheanacho anayekipiga Manchester City ameshinda tuzo ya mchezaji bora anayechipukia

 Alex Iwobi wa Arsenal alitangazwa kuwa kinda bora

 Timu ya taifa ya Uganda  'The Cranes' ikatajwa kuwa ni timu bora ya taifa (wanaume) kwa mwaka 2016

Mabingwa wa Afrika, Mamelodi Sundowns wakaibuka kuwa klabu bora barani Afrika 2016

Timu ya taifa ya Nigeria ilitwaa tuzo ya timu bora (wanawake) mwaka 2016

 Kocha mkuu wa Sundowns ndiye kocha bora mwaka 2016


 Mnigeria Asisat Oshoala ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa upande wa wanawake

Mwamuzi bora ni Bakary Papa Gassama

Na hiki hapa ndicho kikosi bora cha Afrika mwaka 2016

Post a Comment

 
Top