BOIPLUS SPORTS BLOG

LIBRE VILLE, Gabon

TIMU ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imepangwa kundi moja na vinara wa soka ukanda wa Afrika Mashariki Uganda katika michuano ya kufuzu Kombe la mataifa Afrika mwaka 2019.

Stars ambayo itakuwa chini ya kocha wa muda Salum Mayanga imepangwa kundi L sambamba na Uganda, Lesotho na Cape Verde huku kukionekana na ahueni endapo itachanga karata zake vizuri.

Kwa upande wa timu ya Taifa ya Kenya 'Harambee Stars' ambayo ipo ukanda huu wa Afrika Mashariki imepangwa kundi F sambamba na Ghana, Ethiopia na Sierra Leone.

Wenyeji wa michuano hiyo timu ya Cameroon ambayo imefuzu moja kwa moja imepangwa kundi B pamoja na timu za Morocco, Malawi na mshindi kati ya Comoro na Mauritius.

Wakati huo huo timu za Sao Tomé, Madagascar, Comoro, Mauritius, Djibouti na Sudan Kusini wataanzia kwenye mechi za mtoano mwezi Machi ambapo Mataifa matatu yataingia kwenye hatua za makundi.


Jinsi Makundi yalivyopangwa:

Kundi A: Senegal, Equatorial Guinea, Sudan, Sao Tome/Madagascar

Kundi B: Cameroon, Morocco, Malawi, Comoro/Mauritius

Kundi C: Mali, Gabon, Burundi, Djibouti/Sudan Kusini.

Kundi D: Algeria, Togo, Benin Gambia.

Kundi E: Nigeria, Afrika Kusini, Libya, Shelisheli.

Kundi F: Ghana, Ethiopia, Sierra Leone, Kenya.

Kundi G: DR Congo, Congo Brazzaville, Zimbabwe, Liberia.

Kundi H: Ivory Coast, Guinea, Jamhuri ya Afrika ya kati, Rwanda.

Kundi I: Burkina Faso, Angola, Botswana, Mauritania.

Kundi J: Tunisia, Misri, Niger, Swaziland.

Kundi K: Zambia, Msumbiji, Guinea-Bissau, Namibia.

Kundi L: Cape Verde, Uganda, Tanzania, Lesotho.

Post a Comment

 
Top