BOIPLUS SPORTS BLOG


Mwandishi Wetu, Zanzibar
SIMBA imeendelea kuangusha moja moja baada ya leo kuwazamisha KVZ kwa bao 1-0 lakini safari ya kuelekea nusu fainali ya kombe la Mapinduzi ikiendelea kama kawaida.

Bao pekee katika mchezo huo ulioanza majira ya saa 2:15 usiku huu kwenye uwanja wa Aman liliwekwa nyavuni na Mzamiru Yassin dakika ya 44 akimalizia kiulaini mpira ambao walinzi wa KVZ walidhani ni wa kuotea.

Huu ni mchezo wa pili kwa Simba ambao awali walipata ushindi kama huu dhidi ya Taifa Jang'ombe hivyo sasa wanafikisha alama sita na mabao mawili tofauti na watani zao Yanga ambao walianza michuano hiyo kwa kutoa dozi nzito ya mabao 6-0 kwa Jamhuri.

Dakika ya 89 KVZ walipata pigo baada ya mlinzi wao Rashid Omar Rashid kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kufuatia kumvuta jezi Said Ndemla aliyekuwa amemzidi kasi huku akijiandaa kwenda kumsabahi kipa Abdallah Suleiman.

Post a Comment

 
Top