BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu
AZAM FC imeingia mkataba wa miezi sita na kocha mpya kutoka Romania, Aristica Cioaba ambaye tayari yupo visiwani Zanzibar ambako timu hiyo inashiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Cioaba ameingia mkataba huo mfupi akichukua nafasi ya Mhispania Zeben Henerndez ambaye walifikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo.

Ciaoba amesaini mkataba huo mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Azam FC, Saady Kawemba ambao makubaliano yake ni kuongeza mara baada ya msimu kumalizika. Kocha huyo huenda akawepo kwenye benchi la ufundi wakati wa mchezo wa nusu fainali za michuano hiyo ambapo Azam itacheza na Taifa Jang'ombe muda mfupi ujao.

Post a Comment

 
Top