BOIPLUS SPORTS BLOG

LIBREVILLE, Gabon
Langa Lesse Bercy

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limetoa nafasi ya mwisho kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Jamhuri ya Kidemokrasia Congo (FECOFOOT) kumpeleka mchezaji Langa Lesse Bercy jijini Libreville, Gabon kwa ajili ya kipimo kipya cha MRI ili kutambua umri wake halisi.

CAF limetaka FECOFOOT kumpeleka mchezaji huyo ndani ya siku 10 zijazo kuanzia jana Januari 12.

CAF  ilimwita mchezaji huyo mara mbili mwaka jana lakini FECOFOOT ilishindwa kumpeleka kwa sababu mbalimbali wanazozijua huku ikionekana kuwa mchezaji huyo umri wake ni mkubwa.

Bercy alilalamikiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwamba amezidi umri hivyo kuhitajika kumpeleka CAF kufanyiwa vipimo vya MRI kwani hakustahili kucheza hatua ya kufuzu kwa michuano hiyo ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana.

Fainali za vijana zinatarajiwa kufanyika katika nchi nyingine itakayotangazwa hapo baadaye baada ya Madagascar kuondolewa kuandaa kutokana na kubainika kutokamilisha baadhi ya taratibu.

Shirikisho hilo limefungua milango kwa kwa nchi wanachama wengine kuandaa fainali hizo ambapo Mwisho wa kupokea maombi ni Januari 30.

Post a Comment

 
Top