BOIPLUS SPORTS BLOG


UNITED YAMTENGEA DAU GRIEZMANN
Klabu ya Manchester United imeamua kumfungia kazi mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann ili kupata saini yake.

Kocha wa United Jose Mourinho anataka kuongeza nguvu katika idara ya ushambuliaji na Griezmann akiwa chaguo la kwanza katika nyota  anaowataka Old Trafford licha ya mshambuliaji huyo kukiri kutaka kubaki Atletico.

United wamemtengea mshahara wa paundi 220,000 kwa wiki endapo atakubali na kutua kwa Mashetani hao.


GUANGZHOU WAMTAKA MESSI

Baada ya klabu ya Guangzhou Evergrande ya China kushindwa kumshawishi mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo sasa wamehamishia nguvu kwa Lionel Messi.

Timu hiyo imeanda ofa ya euro milioni 250 kwa Barcelona kama ada ya uhamisho huku ikitaka kumlipa Messi mshahara wa euro milioni 78 kwa mwaka na hela ya ziada ya euro 125000 kwa goli au pasi ya mwisho atakayotoa.

Huenda Messi akakataa ofa hiyo kwani bado yupo katika kiwango bora na angependa kumalizia soka lake Barcelona inawa ofa hiyo ni ya kutamanaisha.


ZIDANE ASEMA PEPE HAONDOKI

Kufuatia tetesi zinazomuhusisha beki wa kati wa Real madrid Pepe kutimkia China au Manchester United kocha wa timu hiyo Zinedine Zidane amekana taarifa hizo.

Madrid itamruhusu Pepe kuondoka klabuni hapo kama itapata mbadala wake katika majira ya joto ya usajili lakini timu kutoka China iliandaa mshahara wa euro milioni 10.

Madrid imekataa ofa zote kwa muda huu na pia beki huyo hajaingia katika mazungumzo na klabu zinazo muhitaji kwa sasa.


AUBAMEYANG ATENGEWA DAU CHINA

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick Aubameyang ameandaliwa ofa nono na klabu kutoka nchini China.

 Baada ya Carlos Tevez,Oscar na Mikel Obi  kujiunga katika klabu za China sasa imefikia zamu ya Aubameyang ambaye ametengewa dau la paundi milioni 150.

Dortmund imekataa taarifa ya kuwa imepokea dau hilo ambapo Aubameyang alikiri kutaka kutimkia Real Madrid.

Post a Comment

 
Top