BOIPLUS SPORTS BLOG

BARCELONA, REAL WAMTAMANI DELE

BAADA ya kiungo wa Tottenham Hotspur Dele Alli kuonesha uwezo mkubwa hivi karibuni miamba ya soka ya Hispania Real Madrid na Barcelona wamemtolea macho kijana huyo wakionyesha wazi nia yao ya kumtwaa.


Dele ambaye ana miaka 20 amekua katika kiwango bora huku akifunga magoli mawili mawili katika mechi tatu za mwisho alizocheza. Muingereza huyo ambaye anafananishwa na wakongwe kama Gerrard na Lampard huenda akashawishika na kujiunga na klabu hizo huko mbeleni.

Spurs wameweka dau la paundi milioni 50 endapo klabu yoyote itahitaji saini yake na kumruhusu kiungo huyo atimke White Hart LaneEVRA AACHWA KATIKA KIKOSI CHA JUVENTUS KISA MAN UNITED


Beki wa Kushoto wa Juventus Patrice Evra ameachwa katika kikosi cha Juventus kitakachokipiga na Bologna baada ya kuhusishwa na Man United


Taarifa kutoka Calciomercato inasema Evra ameachwa baada ya kufikiria kurudi United na huenda wiki hii akawa amefanya maamuzi juu ya mstakabari wake klabuni Juventus.


Evra ambaye alijiunga na Juventus akitokea United majira ya joto hapo 2014 kwa uhamisho huru amepata na shauku kurejea katika klabu yake hiyo ya zamani.AC MILAN WAANDAA DAU LA USAJILI


Miamba ya soka ya Italia AC Milan inaanda dau la usajili ili kuweza kuboresha kikosi chake kilicho chini ya kocha Vincenzo Montella


Huyo ni kufuatia kauli ya kocha huyo kuwa hajavutiwa na klabu kubwa kama Milan kutocheza michuano mikubwa ya klabu kama klabu bingwa barani Ulaya ukiachilia mbali ukubwa wa klabu hiyo.


La Gazetta inaripoti kuwa Bodi ya Milan imeamua kumtengea dau la euro 150 milioni kwa ajili ya usajili wa wachezaji kama Domenico Berardi, Federico Bernardeschi, Keita Balde Diao na Mateo Musacchio ambao wameonesha nia ya kuwahitaji ili kuboresha kikosi chao.MANCHESTER CITY WAMTAKA BASTUBER


Beki wa kati wa Bayern Munich Holger Badstuber amehusishwa na klabu ya Manchester City kufuatia kutokuwa na nafasi katika klabu ya Bayern Munich.


Kocha wa City amekiri kuwa wanafikiria swala hilo kwa karibu akizungumza na vyombo vya habari alisema "tunafikiria kuongeza beki mmoja, namfahamu Holger ni mchezaji mzuri sana ila ni mchezaji wa Bayern.Tunatakiwa kwanza kuongea na Bayern alafu tuzungumze na Holger"


Holger ambaye hajapewa ofa ya mkataba mpya hapo Bayern huku akiwa apati nafasi ya kutosha klabuni hapo huenda akavutiwa na ofa ya City endapo itawekwa mezani.LEWANDOWSKI AIKATAA OFA KUTOKA CHINA


Mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich na Raia wa Poland Robert Lewandowski ameikataa ofa ya klabu moja ya China ambayo ingeweza kumfanya mchezaji huyo kuwa anayelipwa zaidi kuliko wachezaji wote duniani.


Wakala wa mshambuliaji huyo Cezary Kucharski amethibitisha kuwa Lewandowski alitengewa ofa kubwa zaidi ya aliyopewa Tevez huko Shanghai. Klabu kutoka China zimekuwa zikitoa ofa mbalimbali kubwa kwa ajili ya wachezaji mahiri barani Ulaya


Cezary Kucharski Alisema "kama Lewandowski angelikubali kutimkia China mshahara wake ungekuwa zaidi ya euro 40 milioni ambayo ni zaidi ya anayolipwa Carlos Tevez". Lewandowski ameamua kubakia Bayern Munich na kuendelea kuwapata kile mashabiki wa Bavarians wangependa kukipata kutoka kwake.MASTAA WA EPL WAHITAJIKA CHINA


Kufuatia usajili wa Mikel Obi, Oscar na Carlos Tevez kujiunga na klabu za uko China, imefikia wakati wa klabu hizo za China zimeandaa ofa kubwa zaidi kwa ajili ya mastaa wa ligi kuu nchini Uingereza


Wachezaji kama Dele Alli, Harry Kane, Ross Barkley na Daniel Sturridge wameandaliwa ofa kubwa zaidi kuweza kushawishika na kutimkia China. Klabu hiyo ya China imeanda mshahara wa paundi 800,000 kwa wiki kwa wachezaji hao


Kumekuwa na ofa kubwa zikitolewa na klabu hizo za China uku mastaa kama Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Lewandowski wakiwa wameshazikataa.


Imeandaliwa na Abra David Jr kupitia mitandao barani Ulaya.

Post a Comment

 
Top