BOIPLUS SPORTS BLOG

RAKITIC KUJIUNGA NA MAN CITY

Kiungo mshambuliaji wa Barcelona Ivan Rakitic anatarajiwa kujiunga na Manchester City kufuatia kushindwa kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha FC Barcelona.

Taarifa kutoka Hispania na Croatia zinasema Rakitic ambaye mkataba wake unaisha mwaka 2019 hajapewa maboresho huku akiwa na nafasi ndogo kuanza katika timu hiyo.

Rakitic amekua akisifiwa na kocha wa City Pep Guardiola na kuonesha nia ya kumhtaji kiungo huyo klabuni hapo.


DROGBA KURUDI MARSEILLE

Mshambuliaji wa klabu ya Montreal Impact Didier Drogba amefungua milango ya kutaka kurudi katika klabu yake ya zamani ya Olympic Marseille ya Ufaransa baada ya  kumaliza mkataba wake na timu hiyo inayoshiriki ligi ya Marekani.

Drogba alisema "ningependa kurejea Marseille siku moja na kuthibitisha ahadi yangu,ila kwa sasa napata kipato kizuri na kurudi Ufaransa itabidi mshahara wangu upungue mara mbili na hamna mtu anaependa kufanya kazi na kulipwa pungufu ila nisiporudi watasema siipendi".


INTER, UNITED ZAINGIA VITANI KWA  MANOLAS

Beki wa kati wa AS Roma Kostas Manolas amezivutia klabu za Manchester United na Inter Milan ambazo zimeonesha nia ya kutaka kumsajili nyota huyo raia wa Ugiriki.

Manolas 25 amekuwa mchezaji muhimu kwa Roma kutokana na kiwango bora alicho nacho kwa sasa ambapo miamba hiyo ya Italia wanataka dau la paundi milioni 50 ili waweze muachia Mgiriki huyo huku United ikiandaa ofa ya paundi milioni 47 na Inter  wakiwa bado hawajaanda ofa yoyote mpaka sasa.


ZAZA KUTIMKIA FIORENTINA

Baada ya mchezaji wa Fiorentina Nikola Kalinic kuhusishwa na dili la kuelekea China klabu ya hiyo inajiandaa na kumtaftia mbadala wake ambaye ni Simon Zaza.

Fiorentina wanajiandaa na ofa ya paundi milioni 15 ili kuweza kumnyakua mshambuliaji huyo wa West Ham United.

Zaza amekuwa akihama hama na kucheza muda mfupi katika klabu alizowahi kuzitumikia kutokana na kushindwa kufanya vizuri.


DORTMUND BADO WANAMTAKA ZELALEM

Klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani haijakata tamaa katika mchakato wa kupata saini ya kinda wa Arsenal Gedion Zelalem 

Kinda huyo anafikiria kutimka klabuni hapo baada ya kutopata nafasi za kutosha chini ya kocha Arsene Wenger.

Dortmund imeamua kusubiri hadi mwisho wa msimu wa 2016/17 ambapo Zelalem atakuwa kamaliza mkataba na Arsenal hivyo kumpata akiwa  mchezaji huru.


STOKE CITY WAMTAKA BERAHINO

Baada ya mshambuliaji wa West Bromwich Albion Saido Berahino kupitia kipindi kigumu katika maisha yake ya soka huenda akaamua kujiunga na Stoke City ambayo imeonyesha nia ya kuhitaji saini yake.

Taarifa kutoka Sky Sports inasema kuwa Stoke wameandaa ofa kwa ajili ya mshambuliaji huyo ambayo haijawekwa wazi ila inasemekana ni chini ya ofa ambayo Tottenham Hotspurs walitenga msimu uliopita ya paundi milioni 20.

Post a Comment

 
Top