BOIPLUS SPORTS BLOG

JAMES AKATAA OFA ZA CHINA

Kiungo Mshambuliaji wa Real Madrid James Rodriguez amejiunga katika orodha ya wachezaji waliokataa ofa kutoka klabu za China katika dirisha hili la usajili.

James amehusishwa na taarifa za kutaka kutimka Madrid baada ya  kutengewa ofa mara kumi ya mshahara kwa wiki ambao atalipwa na klabu ya Hebei China.

Wakala wake Jorge Mendes amesema mchezaji huyo hatoondoka Madrid na atamsaidia katika mafanikio yake klabuni hapo.


DAHOUD HAONDOKI JANUARY

Kiungo wa Borussia Monchengladbach Mahmoud Dahoud hatoruhusiwa kuondoka klabuni hapo katika dirisha la usajili la Januari hii.

Mkurugenzi wa klabu hiyo Max Eberl aliweka bayana kuwa hawapo tayari kumuuza kiungo huyo kwa sasa kwani bado ni muhimu na hawafikirii kumuuza hivi takaribuni.

Dahoud amehusishwa na kutaka kujiunga na klabu ya Liverpool ambayo imekuwa ikimfuatilia kwa muda mrefu huku Juventus ikijiunga katika kinyang'anyiro hicho.


BRANDT AIVUTIA LIVERPOOL

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameonyesha kuvutiwa na uwezo wa kiungo mshambuliaji wa Bayern Leverkusen Julian Brandt na anataka kumsajili kwenye timu yake.

Klopp amekua akitafuta kiungo mshambuliaji ambaye atasaidia Liverpool katika safu ya ushambuliaji baada ya Sadio Mane kujiunga na timu yake ya Taifa ya Senegal kwenye michuano ya Kombe la mataifa barani  Afrika itakayofanyika nchini Gabon.

Haitokuwa kazi rahisi kwa Liverpool kumtwaa Brandt kwani klabu za  Bayern Munich na Manchester United zimeonyesha nia za kumshawishi kijana huyo kujiunga nao.


GAITAN AITAKA EPL

Baada ya Kiungo wa klabu ya Atletico Madrid Nicolas Gaitan kushindwa kupata nafasi kwenye kikosi hicho chini ya kocha cha Diego Simeone amefikiria ofa za kutoka ligi ya Uingereza ili kupata nafasi zaidi.

Klabu za Manchester United, Man City na Tottenham Hotspurs zimeonesha nia ya kumuhtaji kiungo mshambuliaji huyo aliyejiunga na Atletico akitokea Benfica kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 21.

Spurs inataka kumsajili Gaitan kwa mkopo hadi Juni ikiwa na nafasi ya kumsajili moja kwa moja baada ya kumalizia kwa mkopo huo.VALENCIA WAMTAKA JESE

Klabu ya Valencia ya Hispania imekuwa klabu ya mwisho kuonyesha nia ya kumsajili winga wa Paris Saint Germain Jese Rodriguez

Jese ambaye amekuwa na wakati mgumu PSG tangu ajiunge akitokea Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa euro milioni 25 katika mkataba wa miaka mitano ambapo usajili wa Julian Draxler umemfanya kuona nafasi yake inazidi kuwa ndogo klabuni hapo.

Valencia watakuwa wakishindana na klabu za Liverpool na West Ham ambazo pia zinataka saini ya winga huyo.


ROMA WAMTAKA KINDA WA CHELSEA

Baada ya Chelsea kumrejesha kinda wake Charly Musonda kutoka Real Betis alipokuwa kwa mkopo ameshindwa kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza.

AS Roma imeamua kuchukua nafasi hiyo ili kumsajili winga huyo kufanya maboresho kwenye kikosi hicho huku akitakiwa kuziba pengo lililoachwa na Mohamed Salah aliyejiunga na timu ya Taifa ya Misri kwenye michuano ya AFCON nchini Gabon.

Musonda anakua chaguo la tatu la Roma kama dili la kuwasajili Soufiane Feghouli na Deulofeu yakiwama watachukua nafasi hiyo kumnyakua kinda huyo wa Chelsea.

Imeandaliwa na Abra David Jr kupitia mitandao ya barani Ulaya

Post a Comment

 
Top