BOIPLUS SPORTS BLOG

www.boiplus.blogspot.com
RONALDO AMSHAWISHI JAMES KUBAKI MADRID

Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amemshawishi mchezaji mwenzake James Rodriguez kubaki klabuni hapo na kusitisha mpango wa kuondoka katika dirisha hili la usajili.

James ambaye alikuwa anafikiria kutimkia kwa vinara wa ligi ya Uingereza Chelsea mwezi huu amesitisha mpango huo na kuamua kuitumikia miamba hiyo ya soka ya Hispania.

James amekuwa hana uhakika wa namba chini ya kocha Zinedine Zidane ingawa amekuwa na msaada katika timu hiyo ikiwa anaongoza kutoa pasi za mwisho za magoli tisa sambamba na Tonny Kroos huku akifunga mabao manne katika msimu 2016/17.


PAYET KUJIUNGA NA CHELSEA

Kufuatia klabu ya West Ham United kutoa taarifa  kuwa kiungo wao mshambuliaji Dimitri Payet kagoma kuichezea tena timu hiyo mahasimu wao Chelsea wameonesha nia ya kumtaka kumsajili mchezaji huyo.

Kitendo cha Payet kugoma kinaelezwa ni kutokana na klabu hiyo kukataa ofa ya paundi milioni 20 iliyotolewa na Paris Saint Germain ya Ufaransa.

Kocha wa Chelsea Antonio Conte anavutiwa na kiwango cha kiungo huyo raia wa Ufaransa na anaweza akamnasa katika dirisha hili la usajili.


JUVENTUS KUMNASA KOLASINAC

Miamba ya soka ya Italia Juventus ipo katika hatua za mwisho kumalizia dili la kumnasa beki wa kushoto wa Schalke 04 Sead Kolasinac.

Juventus imeamua kumsajili beki huyo  baada ya beki wake wa kushoto Patrice Evra kuhusishwa na kutaka kurejea  klabu yake ya zamani  Manchester United au Valencia.

Evra ambaye alikiri kufikiria kurejea United ameifanya Juventus kukaa katika hali ya kujiandaa na kukosa huduma yake huku wakimwacha katika mechi iliopita ya ligi dhidi ya Bologna.

Kolasinac huenda akajiunga na Juventus mwezi Juni baada ya mkataba wake na Schalke kumalizika.


MULLER AFIKIRIA KUIKACHA BAYERN

Mshambuliaji wa Bayern Munich Thomas Muller ameweka wazi kufikiria ofa zitakazokuja kwa ajili yake kufuatia kutofurahishwa na hali ya kuwekwa benchi mara kwa mara.

Muller alisema "Mechi ya mwisho dhidi ya RB Leipzig ilikua nicheze kutokana na mazingira sikucheza sijisikii vizuri kukaa benchi".

Muller amekuwa mchezaji tegemeo kwa muda mrefu sasa kwenye kikosi cha Bayern lakini amejikuta katika wakati mgumu chini ya kocha Carlo Ancelotti baada ya kuanza kuwekwa benchi katika michezo mbali mbali.

Imeandaliwa na Abra David Jr kupitia mitandao mbalimbali barani Ulaya

Post a Comment

 
Top