BOIPLUS SPORTS BLOG


MESSI KUTIMKA  BARCELONA

Nyota wa FC Barcelona Lionel Messi huenda akafikiria ofa kutoka kwa klabu nyingine baada ya miamba hiyo ya Hispania kuchelewa kumpa mkataba mpya.

Timu za Chelsea, Manchester United na Man City ni miongoni mwa klabu  zinzazo fuatilia kwa karibu  hali ya mkataba wa Messi na Barcelona huku wakiangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji huyo raia wa Argentina.

Messi ana mkataba wenye thamani ya paundi milioni 250 huenda akaondoka kama mchezaji huru kama asipoongeza mkataba na kuamua kutimkia katika ligi kuu ya Uingereza.

COSTA ATOFAUTIANA NA CONTE

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa ameachwa katika kikosi kitakachocheza na  mabingwa wa ligi ya Uingereza timu Leicester City leo katika dimba la Kings Power baada ya kutofautiana na Kocha wake Antonio Conte.

Costa ameachwa kufuatia kutupiana maneno makali na kocha wake juu ya utarartibu wa mazoezi waliokuwa wanapewa ambapo amekuwa akilalamika kuwa yanamletea maumivu katika misuli na kutaka kupumzishwa katika mechi kadhaa hali iliomfanya Conte ampumzishe kwenye mchezo wa leo.

Mbali na sababu hizo Costa amevutiwa na ofa kutoka klabu Tianjin Quanjin ya China ambayo itamlipa mshahara wa paundi 570,000 kwa wiki.

INTER  WATUMA OFA KWA VERRATTI

Inter Milan ya Italia imetuma ofa ya euro milioni 78 Paris Saint Germain kwa ajili ya kuhitaji huduma ya kiungo  wake Marco Verratti.

Wakala wa Verratti Donato Di Campli alisema "Verratti anafuraha klabuni hapa ila katika soka hatochezea Ufaransa pekee bali na ligi nyingine".

Verratti ambaye anamaliza mkataba wake mwaka 2018 huenda PSG wakakubali ofa hiyo ili kupata faida ya euro milioni 11 ukilinganisha na ada ya uhamisho waliomsajilia kiungo huyo kutoka Pescara.

JUVE WAMNYATIA LALLANA

Klabu ya Juventus ya Italia ipo kwenye mikakati thabiti ya kuhakikisha inamsajili kiungo mshambuliaji wa Liverpool Adam Lallana kufuatia kiwango kizuri chini ya Kocha Jurgen Klopp.

Lallana ameifungia Liverpool mabao saba na kutoa pasi saba za mwisho msimu huu amesababisha klabu PSG na Barcelona kuhitaji saini yake pia.

Barcelona ambayo inajiandaa kumuacha Ivan Rakitic huenda ikamsajili Lallana kama mbadala wake huku PSG ikiongeza nguvu kwa kiungo huyo baada ya kumuweka sokoni winga wao Jese Rodriguez.

CARRASCO KUMRITHI CAZORLA ARSENAL

Klabu ya  Arsenal inajiandaa kutafuta mrithi wa kiungo Santi Cazorla ambae umri wake unamtupa mkono pia na uwezo wake ukipungua kutokana na majeruhi ya mara kwa mara huku jicho lao likiwa kwa nyota wa Atletico Madrid Yannick Carrasco.

Carrasco ameifungia Atletico mabao  10 katika mashindano yote lakini itawawia vigumu Arsenal kuishawishi timu hiyo kumuuza kiungo huyo kwani amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu chini ya kocha Diego Simeone.

Arsenal itawalazimu kutoa kiasi kikubwa cha fedha ili Atletico wamuachie kiungo huyo mshambuliaji ambaye ana mkataba  wenye thamani ya paundi milioni 85.

Post a Comment

 
Top