BOIPLUS SPORTS BLOG

MORATA KURUDI JUVENTUS

Mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata huenda akafikiria kurejea timu yake ya zamani ya Juventus baada ya kushindwa  kupata nafasi ya kutosha kwa miamba hiyo ya Hispania.

Morata  amekua chaguo la pili baada ya Karim Benzema anahitaji kupata nafasi zaidi  chini ya Kocha Zinedine Zidane  ili aweze kupata nafasi ya kuitwa timu ya taifa ya Hispania.


WEIGL HAONDOKI DORTMUND

Wakala wa kiungo wa Borusia Dortmund Julian Weigl, Michael Decker ametoa kauli ya kuwa mchezaji huyo hataondoka klabuni hapo licha ya  kuhusishwa na kutaka kujiunga na timu mbalimbali barani Ulaya.

Weigl amesaini mkataba mpya na Dortmund utakao muweka klabuni hapo hadi mwaka 2021 huku timu yake ikisema haiko tayari kumruhusu kuondoka.


CHELSEA KUMNASA RODRIGUEZ

Chelsea wapo katika nafasi nzuri ya kumsajili beki wa kushoto wa timu ya Wolfsburg ya Ujerumani Ricardo Rodriguez kwa mujibu wa gazeti la The Sun.

 Chelsea wamefanya mawasiliano na wawakilishi wa beki huyo wa kushoto mwenye miaka 27 huku wakitegemea  kumaliza dili hilo la paundi milioni 21 katika dirisha hili la usajili.


PJANIC KUTUA ARSENAL

Klabu ya Arsenal inajianda kutoa ofa ya kumnasa kiungo wa Juventus Milarem Pjanic.

Kiungo huyo alitua Juventus majira ya joto yaliopita anatazamiwa kuwa mrithi wa Santi Cazorla ambaye amekua akipatwa na majeraha mara kwa mara.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ameishauri bodi ya klabu hiyo ijiandae kutoa kitita cha paundi milioni 28 ili kumpata kiungo huyo mbunifu katika dirisha hili la usajili


GRIEZMANN KUBAKI ATLETICO MADRID

Mshambuliaji hatari wa klabu ya Atletico Madrid Antoine Griezmann  huenda akabakia klabuni hapo kwa muda mrefu zaidi baada ya kutoa kauli juu ya kuhusishwa kuondoka kwa miamba hiyo ya Hispania.

Griezmann amehusishwa na kujiunga na timu Manchester United, Chelsea na Paris Saint Germain amewahakikishia mashabiki wa Atletico kubakia klabuni hapo akiwajibu waandishi wa habari alisema "sipendi swali hilo lijirudie tena nina furaha hapa na sitaki kujua ya mbeleni najali ya sasa kucheza mbele ya mashabiki hawa wa Atletico".


MARSEILLE WAMFUKUZIA SCHNEIDERLIN

Baada ya kocha wa Manchester United Jose Mourinho kutoa baraka kwa kiungo Morgan Schneiderlin kutimka kama akipata ofa nzuri kutoka klabu mbalimbali.

Timu za Juventus, Everton, Paris Sainy Germain na Olympic Marseille wameingia katika kinyang'anyiro hicho cha kumnasa kiungo huyo baada ya taarifa ya kukataliwa ofa ya paundi milioni 19 kutoka kwa Everton.

Marseille wanahtajika kupeleka dau la paundi milioni 24 ambayo klabu ya Man Utd ipo tayari kupokea kiasi hicho.

Post a Comment

 
Top