BOIPLUS SPORTS BLOG

MADRID KUMNASA ANDRE SILVA
Mshambuliaji chipukizi wa FC Porto ya Ureno Andre Silva huenda akajiunga na miamba ya soka ya Hispania Real Madrid katika majira ya joto mwezi Juni.

Silva amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu ambapo  ameivutia pia klabu ya Arsenal na lakini miamba hiyo ya Hispania inapewa nafasi kubwa ya kumnyakua mchezaji huyo.

Taarifa zinasema kuwa Madrid imefikia makubaliano na Porto kwa ada ya uhamisho wa euro milioni 58 na kwa ajili ya Silva.

LIVERPOOL YAMFUNGIA KAZI PROMES

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amependekeza nyota wa Spartak Moscow Quicy Promes kuwa moja ya wachezaji ambao angependa kuwasajili mwezi huu  ili kuziba nafasi ya Sadio Mane.

Mane ameondoka Liverpool kwa ajili  kuiwakilisha nchi yake ya Senegal kwenye michuano ya mataifa barani Afrika itakayoanza wiki ijayo nchini Gabon hivyo kuacha pengo katika nafasi ya ushambuliaji.

Liverpool inategemea kupeleka dau la paundi milioni 25 ili  kumnyakua mshambuliaji huyo.


CHELSEA WAANDAA DAU LA ROMAGNOLI

Baada ya kocha wa Chelsea Antonio Conte kuhamia katika mfumo wa 3-4-3 inamfanya kutafuta beki mwengine atakae endana na mfumo huo katika muendelezo wa kupata matokeo mazuri.

Chelsea wamehusishwa na Alessio Romagnoli katika dirisha hili la usajili na wanategemewa kupeleka ofa mapema ili waweze kumpata beki huyo.Chelsea inajiandaa na ofa ya paundi milioni 49 ambayo wanategemewa itapokelewa na AC Milan

Mbali na Rogmanoli Chelsea pia inafuatilia mwenendo wa mkataba wa beki wa Real Madrid Pepe ambaye hajasaini mkataba mpya na miamba hiyo ya soka ya Hispania.

  KIMPEMBE AZITOA MATE KLABU ZA UINGEREZA 

Klabu ya Paris Saint Germain inajianda na jitihada za kumbakisha mchezaji chipukizi Kimpembe Presnel ambaye ameonesha uwezo mkubwa akiwa na matajiri hao wa Ufaransa.

Kimpembe amefanya kazi kubwa akiwa na PSG iliowafanya klabu kama Chelsea, Manchester United na Liverpool kumtolea macho na kujiandaa na mikakati ya kumnyakua mchezaji huyo

Kimbembe amekua akitumiwa sana na kocha Unai Emery na kumfanya pia afikiriwe katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa.BAYERN  KUWAPIKU UNITED KWA SEMEDO

Baada ya taarifa kuenea kuwa klabu ya Manchester united ipo mbioni kumnasa beki wa Benfica Nelson Semedo hali imekua tofauti mara baada ya Bayerm Munich kuingilia kati dili hilo.

Semedo ambaye amekuwa na msimu mzuri Benfica amezivutia klabu hizo na kuzifanya kuingia katika king'anyiro cha saini yake ambapo watatakiwa kulipa mkataba wenye thamani ya euro milioni 60.

Bayern wapo tayari kutoa euro milioni 40 na kuwapiku  United kama ilivyokuwa kwa  Renato Sanchez kutika majira ya joto yaliopita.

Post a Comment

 
Top