BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu

MABINGWA watetezi wa Kombe la Mapinduzi, URA kutoka Uganda imeanza vizuri michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KVZ, mechi hiyo imechezwa Uwanja wa Amani, visiwani Zanzibar.

KVZ walicheza vizuri kipindi cha kwanza nakufanya mashambulizi mengi langoni mwa URA lakini walishindwa kufunga huku Waganda hao wakicheza kwa tahadhari kubwa.

Mshambuliaji Labama Bogota alipeleka kilio kwa Wazanzibar hao baada ya kufunga mabao yote mawili kutokana na kuwazidi ujanja mabeki wa KVZ.

Hata hivyo kiwango cha mabingwa hao kimetia shaka uwezo wa kutetea ubingwa wao hasa uwepo wa timu za Simba,Yanga na Azam FC kutoka bara ambao wanaonekana kujipanga vizuri hasa uimara wa vikosi vyao.

Simba na Yanga ambazo zipo nafasi mbili za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom zinatajwa kuwa miongoni mwa timu zitakazofanya vizuri kutokana na ushindani wanaounyesha kwenye VPL huku wakichagizwa na uwepo wa makocha wao Joseph Omog raia wa Cameroon anayeifundisha Simba na Mzambia wa Yanga, George Lwandamina.

Post a Comment

 
Top