BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu, Njombe
Ofisi za Chama Cha Soka Mkoa wa Njombe (NJOREFA)

UCHAGUZI Mkuu wa Chama cha soka mkoa wa Njombe (NJOREFA) unatarajiwa kufanyika Januari 29 na tayari wajumbe wamechukuwa fomu za kugombea nafasi mbalimbali na kufanyiwa usaili.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa leo Ijumaa na Kamati ya Uchaguzi ya chama hicho ni kwamba kesho 
na keshokutwa ni siku ni pingamizi pamoja na kukata rufaa kwa wagombea ambao kwa namna moja au nyingine hawajakidhi vigezo.

Kamati hiyo imeeleza kuwa Januari 17 zitasikilizwa rufaa hizo huku Januari 23 majina yote ya wagombea yaliyopitishwa yatawekwa hadharani na wakati kampeni zitaanza Januari 24 hadi 28.

Wagombea waliochukua fomu na nafasi zao ni Stanley Lugenge, 
Yono Kevela na Stanley Njowoka (Mwenyekiti), Emmanuel Mbogela (Makamu Mwenyekiti), Filotrus Mligo na Vincent Majili (Katibu Mkuu).

Nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Lwimiko Mbafu, Mwakilishi wa Klabu ni Brown Mlyuka, Abubakar Aziz na 
Erasto Mpete wakati Mwakilishi wa Mkutano Mkuu TFF ni Thobias Sanga, Kisari Aloyceline na Thobias Lingalangala.

Katika uchaguzi huo pia nafasi nyingine zitakazochaguliwa ni Meeka Hazina na Msaidizi wake, Katibu Msaidizi, Mwakilishi mpira wa miguu kwa wanawake ambao bado hawajachukuwa fomu.

Post a Comment

 
Top